Matukio Ziara ya Rais Kikwete Nchini Finland
UHUSIANO baina ya Tanzania na Finland ni wa kudumu na utaimarishwa na kutafutiwa namna ya kuukuza zaidi ya hapa ulipo sasa. Rais Sauli Niinisto wa Finland amemueleza Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 2 Juni, Ikulu, jijini Helsinki wakati wa Mazungumzo baina ya viongozi hao. “Uhusiano wetu ni wa muda mrefu, ni uhusiano ambao umedumu kwa miaka 50, tumekuwa na uhusiano …
Rais Kikwete Akemea Vitisho kwa Wabia wa Maendeleo
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kamwe mahusiano kati ya Tanzania na wabia wa maendeleo hayawezi kutawaliwa na vitisho vya wabia hao wa maendeleo kuikatia Tanzania misaada kwa sababu yoyote ile. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kamwe Serikali yake haiwezi kukubali kudhalilishwa na kuvunjiwa heshima na vitisho hivyo na ikifika mahali Serikali itawaambia wabia …
Kikwete Amteuwa Mkurugenzi Makosa ya Jinai
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani Msuya, kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation). Kabla ya uteuzi huu CP Msuya alikuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai. CP Msuya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Robert S. Manumba ambaye amestaafu kwa mujibu …
Rais Kikwete Ziarani Algiers, Algeria
RAIS was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika. Rais Kikwete amewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria akitokea New …