RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameyataka makampuni na wafanyabiashara wa Marekani kuongeza uwekezaji wao katika Tanzania, akisema kuwa Tanzania inao uwezo wa kupokea zaidi ya mara 10 uwekezaji wa sasa wa makampuni ya Marekani katika Tanzania wa dola za Marekani bilioni 4.5. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania ina uwezo mkubwa zaidi wa kufanya biashara kubwa …