Polisi Wafanikiwa Kukamata Bunduki na Risasi Zilizoibiwa Kituoni Stakishari Dar

JESHI la polisi nchini Tanzania leo limetangaza kupata mafanikio makubwa katika operation maalum inayoendelea ya kuwasaka watu waliohusika katika shambulio la kuvamia kituo cha polisi cha stakshari jijini Dar es Salaam na kuendesha mauaji ya askari wanne wa kituo hicho pamoja na raia waliokua katika kituo hicho huku wakipora kiasi kun]kubwa cha silaha na kutokomea kusikojulikana. Akizungumza na wanahabari muda huu …

DCP Mstaafu wa Polisi Andrew Kumalilwa Azikwa

   Jeneza lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili wake katika Nyumba yake ya Milele. Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa DCP Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mzee Andrew …

Janga Lingine Polisi, Askari Wanyang’anywa Silaha 2

JESHI la Polisi limeendelea kukumbwa na majanga ya askari wake kuvamiwa na kunyang’anywa silaha nyakati za usiku wakiwa kazini. Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya tukio lililotokea mkoa wa Pwani kuvamiwa Kituo cha Polisi na majambazi kuua askari na kupora silaha, Safari hii imetokea mkoani Tanga juzi ambapo askari wawili waliokuwa doria kwa kutumia pikipiki waliporwa silaha mbili aina …

Majambazi Wavamia Polisi, Wauwa Askari na Kuiba Silaha

MAJAMBAZI wasiojulikana idadi yao usiku wa kuamkia leo wamevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani na kuwauwa askari polisi wawili pamoja na kupora silaha adhaa zilizokuwa zimehifadhiwa kituoni hapo. Taarifa zilizotufikia kutoka eneo la tukio zinasema majambazi hao wasiojulikana idadi yao wakiwa na silaha mbalimbali majira ya saa nane kasorobo za usiku wa kuamkia leo walivamia …

Wamachinga Wacharuka, Wavamia Ofisi za Jiji Dar

Na Mwandishi Wetu, WAFANYABIASHARA ndogondogo maarufu kama wa machinga leo jijini Dar es Salaam waliandamana hadi katika Ofisi za Jiji la Dar es Salaam zilizopo eneo la Kamata (mataa) na kuanza kufanya fujo huku wakitupa mawe na kuchoma matairi katika barabara hiyo. Wamachinga hao vijana ambao walikuwa wakifanya fujo hizo huku wakiimba, “..hatukubali, hatukubali, hatukubali…” waliandamana kwa kukimbia toka maeneo …