Wananchi Wamzomea Ofisa Mipango Miji Mkutanoni

Na Mwandishi Wetu, Moshi WANANCHI wa Kijiji cha Uchira Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamemzomea Ofisa Mipango Miji wa Halmashauri hiyo kwenye mkutano wa kijiji ambao ulikuwa kwa ajili ya  kuwataka wananchi wabariki mchoro wa mipango miji wa kijiji hicho kuwa mji mdogo. Mkutano huo ulianza saa tano na nusu na kudumu kwa saa moja kwa malumbano na kupelekea kuvunjika kwa mkutano huo, ambapo …