TGNP Watoa Rambirambi Msiba wa Mwanahabari Kamukara

TGNP Mtandao tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ghafla cha mwanahabari na mhariri Edson Kamukara kilichotokea jioni ya Tarehe 25.06.2015 jijini Dar es salaam. Kutoweka kwake ni huzuni kubwa kwetu, wanahabari na jamii kwa ujumla. Hakika taifa limempoteza mtu makini na mzalendo. Kwa muda mrefu, TGNP Mtandao imefanya kazi na marehemu Kamukara katika kuihabarisha jamii na wanawake wa …