Sababu za Mafuriko Kila Sehemu Dar es Salaam Zatajwa

MVUA zinazoendelea kunyesha nakusababisha mafuriko na hasara kubwa jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini zimetajwa kuwa ni moja ya ushahidi wa udhaifu wa miundombinu ya kweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo ni janga kubwa duniani kwa sasa. Haya yalisemwa na FORUMCC; shirika linalijihusisha na masuala ya mabadiliko ya Tabianchi. Watu zaidi ya 12 wameripotiwa kupoteza maisha mpaka sasa kutokana mafururiko hayo …

Mvua Zaleta Mafuriko Maeneo ya Vijijini Mkoani Kilimanjaro

Mafuriko makubwa yamevikumba vijiji saba kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC na kuathiri miundombinu pamoja na makazi ya watu kujaa maji. Mbunge Lucy Owenya akitembelea maeneo yaliyo athirika na mafuriko hayo. Mbunge Lucy Owenya akitizama sehemu ambayo wananchi walilazimika kuibomoa kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha TPC ili kuruhusu maji kupita. Eneo lililobomolewa ili kuruhusu maji ya mafuriko kupita. …

Hawa Ndiyo ‘Wapuuzi’ Wakazi wa Dar Kipindi cha Mvua…!

MSIMU wa mvua jijini Dar es Salaam wapo baadhi ya watu huvua utu wao na kuvaa mioyo ya wanyama. Hawa hawa huamua kutothamini binadamu wenzao na kuamua kujitamini wao wenyewe. Aina hii ya watu wapo karibu maeneo yote si katikati ya jiji la Dar es Salaam na hata vitongoji anuai. Bila huruma huamua kutiririsha maji maji taka yenye vinyesi kutoka …

Mwananchi- Usifikiri Dampo, ni Kituo Cha Daladala!

Picha ya kwanza, inaonyesha chakula (mapaja ya kuku) kikiuzwa pembezoni mwa kituo cha Mabasi, Banana, wilayani Ilala. Meza zimewekwa juu ya mifereji ya kupitisha Maji ya mvua, ambayo nayo imejaa taka za aina mbalimbali. Picha ya pili ni wakazi wakipita kwa taabu juu ya Maji yenye kinyesi, baada ya baadhi wa wananchi kutumia fursa hii ya mvua kutapisha vyoo! Picha …

Jiji la Dar Bado Limejaa Maji!

Kama picha zinavyoonyesha hapo juu, jiji la Dar limeendelea kutesa wakazi wake kwa madimbwi yaliyosheheni Kila kona baada ya mvua kunyesha. Hapo ni maeneo ya Mayfair Plaza karibu na TMJ Hospital. Ni wakati sasa kwa serikali kuhakikisha jiji(inchi) Ina mifereji endelevu, ili kupunguzia wananchi kadhia hii. Picha zote na Mpiga picha maalum wa dev.kisakuzi.com