Serikali Ichukue Hatua Kupunguza Uhaba wa Dawa

TUNASIKITISHWA na namna ambavyo serikali imekuwa ikishughulikia suala laupungufu wa dawa na vifaa tiba nchini. Siku za karibuni, kumekuwepo na taarifa za ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika sehemu mbalimbali nchinilakini serikali bado haijachukua hatua madhubuti, jambo ambalo linaweza kuchangia wagonjwa kuteseka zaidi na hata kusababisha vifo. Sikika ilitegemea serikali ingeangalia janga hili kwa makini zaidi na kulipa mara …