Magaidi Yahofiwa Kushambulia Michuano ya Euro 2016

TAIFA la Marekani linahofia kwamba huenda michuano ya soka ya Euro 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa mwezi ujao ikashambuliwa na magaidi. Idara ya masuala ya kigeni nchini Marekani imesema idadi kubwa ya watalii wanaotembelea Ulaya katika miezi ya kiangazi huenda pia ikawavutia washambuliji hao hivyo kutoa tahadhari. Michuano ya Euro 2016 inatarajiwa kuandaliwa kuanzia Juni 10 hadi Julai 12, 2016 katika …

VIJANA ARUSHA WANUFAIKA NA ELIMU YA MICHEZO KUTOKA KENYA.

Kituo cha kukuza mchezo wa mpira wa Miguu kutoka nchini Kenya cha Trans Nzoia Youth Sports Association ( TYSA) kimetua Mkoania Arusha na kusaidia baadhi ya watoto ili kuwahamasisha katika mchezo wa Huo. Ofisa wa kukuza michezo katika kituo hicho Francis Ojilo alisema kuwa wameamua kusaidia watoto ili kuhakikisha vijana wanakua na elimu ya michezo pamoja na nidhamu hivyo jamii …

TFF Yataja Tarehe ya Uchaguzi Coastal Union

KAMATI ya Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga utafanyika tarehe 05, Julai 2015. Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Melchesedek Lutema ametoa ratiba ya mchakato mzima wa uchaguzi huo, ambapo tarehe 21-22 Mei mwaka huu zitatangazwa nafasi zote zinazogombewa. Kwa mujibu wa kalenda hiyo …

Mpambano Simba na Yanga Waingiza Mil 427/-

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba iliyochezwa Oktoba 18 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 427,271,000.   Washabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa …