WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuujulisha umma kuwa kivuko cha MV Kilombero II ambacho kilizama tarehe 27 Januari 2016, na kusababisha kusimama kwa hudum ya kivuko kwenye Mto Kilombero Mkoani Morogoro kimeanza kufanyakazi rasmi tarehe 29 Februari, 2016 mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake. Kivuko hicho kinaendelea na ratiba yake ya utoaji huduma ya kivuko kuanzia saa …
Wilaya ya Morogoro Yajivunia Kupunguza Maambukizi ya Malaria
Na Andrew Chimesela, Morogoro HALMASHAURI ya Wilaya ya Morogoro, imefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa asilimia nane (8) ukilinganisha na maambukizi ya ugonjwa huo yalivyokuwa kwa mwaka 2014. Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Dk. Mwanahamisi Yahya ambaye ni Kaimu Mganga wa Kituo cha Afya cha Mkuyuni Wilaya ya Morogoro wakati akiwasilisha taarifa ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa …
Mkuu wa Mkoa Aagiza Sheria Zitumike Kuisafisha Morogoro
Na Andrew Chimesela – Morogoro MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dk. Rajab Rutengwe ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutumia sheria zilizopo katika kusimamia vema suala la usafi wa mazingira. Dk. Rutengwe ametoa agizo hilo 19 Mei, 2015 wakati wa kikao maalum cha uhamasishaji wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira kilichofanyika katika ofisi za mkoa huo. …
Hofu Magaidi; Wapiga Bomu Kijijini Morogoro, Wanne Wajeruhiwa
Na Joachim Mushi, Ifakara HOFU ya watu wanaodhaniwa kuwa magaidi imetanda katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa, kilichopo Wilaya ya Morogoro Vijijini baada ya watu wawili kupiga bomu la kutupa kwa mkono katika kijiji hicho na kujeruhi vibaya watu wanne waliokuwa wakiwadhibiti watu hao. Akizungumzia jana na dev.kisakuzi.com eneo la tukio mmoja wa wanakijiji aliyeshuhudia tukio hilo, Ibrahim Ally mkazi wa …
Maadhimisho Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Kufanyika Morogoro
Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) yatakayofanyika tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu mkoani Morogoro. Na Modewjiblog team Wanahabari na wadau wa habari wanatarajiwa kukutana Mkoani Morogoro kwa siku mbili …