Matapeli Watumia Jina la Mke wa Rais Magufuli ‘Kutapeli’

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefafanua kwamba uchunguzi wao umeonyesha kwamba Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli hana akaunti ya Facebook na tovuti inayohamasisha watu kuomba mikopo ya vikundi vya Vicoba, bali kuna matapeli wa mtandao walifungua akaunti feki ili kutumia jina la mke wa rais. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam Machi 19 na Mkurugenzi Mkuu …