Tanzania Inahitaji Kuendeleza Mipango Miji -Pinda

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania kama nchi inapaswa kuwa na mpango wa kuendeleza mipango miji (master plan) wa nchi nzima unaozingatia ukuaji wa miji yetu. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 10, 2014) wakati akifungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa za Miji kutoka mikoa yote ya …