Wanavijiji Mbeya Walaumiana Udhibiti wa Mimba kwa Wanafunzi

Na Joachim Mushi, Mbeya Vijijini WANAVIJIJI wa vijiji vya Shibolya, Usoha Njiapanda, Simambwe, Ikhoho na Ilembo Usafwa vyote vya wilayani Mbeya Vijijini wametupiana lawama kuhusiana na baadhi ya wazazi na viongozi wa vijiji kuwa wakifumbia macho watu wanaotuhumiwa kuwatia mimba wanafunzi wa msingi na sekondari na kuwakatisha masomo. Kauli hiyo imetolewa juzi na baadhi ya wanakijiji walipokuwa wakifanya mazungumzo na …