Michuano ya RCL Kutimua Vumbi Vituo Vitatu

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoshirikisha timu 27 inaanza kutimua vumbi kesho (Mei 10 mwaka huu) katika vituo vitatu vya Morogoro, Mbeya na Shinyanga kwa mechi mbili kila siku. Kundi A ambalo mechi zake zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, African Sports ya Tanga itacheza na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8 mchana wakati saa 10 …