Wananchi Wamzuia Mgombea Mwenza wa CCM Barabarani Mwanga

BAADHI ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya kuendelea na safari yake. Bi. Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita …