Na K-VIS MEDIA MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umekutana na Wahariri wa vyombo vya Habari Nchini, kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015, kwa nia ya kujitambulisha na kuelezea mikakati yake ya kiutendaji na majukumu iliyo nayo. Akiwasilisha mada kwa Wahariri hao, Mkurugenzi Mkuu wa Kwanza wa Mfuko huo, Masha Mshomba, amesema, Mfuko huo umeanzishwa ili kutekeleza sheria ya fidia …