Coastal Union Yatoa Mchezaji Bora Februari

KIUNGO wa timu ya Coastal Union, Godfrey Wambura amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini. Wambura amechaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya jopo la makocha linalofanya majumuisho ya wachezaji bora wa kila mchezo, ambapo kiungo huyo ameweza kuwapiku wachezaji Saimon Msuva wa Young Africans, Abasirim Chidiebere …