Waziri Mkuu Pinda Asema Mchakato wa Katiba ni Halali na Upo Kisheria

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema mchakato wa Bunge la Katiba unaoendelea hivi sasa ni halali na kwamba mchakato huo ni wa kisheria. Ametoa kauli hiyo Septemba 21, 2014 wakati akizungumza na mamia ya waumini na viongozi mbalimbali waliohudhuria ibada ya uzinduzi wa dayosisi mpya ya Ziwa Tanganyika ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kuwekwa wakfu Askofu Ambele …