Mbunge Adai Kuvuliwa Nguo Bungeni

KUFUATIA vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama, mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo. Mbunge huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua …