Mbunge Joshua Nassar Aanguka na Helkopita…!

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepata ajali baada ya helkopita aliyokuwa akisafiria kupotea mawinguni kabla ya kuanguka na kukwama juu ya miti. Taarifa zilizotufikia zinasema mbunge huyo pamoja na rubani wa helkopita wamekimbizwa kwenye hospitali ya Selian Arusha kwa matibabu zaidi. Mtandao huu utakuletea taarifa zaidi za ajali hiyo baadaye.

Mbunge Atatua Kero ya Maji Kijiji cha Amani Ludewa

Mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe akinywa maji kwa majani ya miti baada ya kuzindua mradi wa maji na kukabidhi vifaa vya kuvuta maji  vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 14.5 kwa wakazi wa kitongoji cha Dodoma kijiji  cha Amani Ludewa  Mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe akisoma maandishi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kitongoji cha Dodoma …

Halima Mdee Apelekwa Segerea, Akosa Dhamana

MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (35), jana alikosa dhamana na kupelekwa rumande katika Gereza la Segerea hadi leo maombi ya dhamana yake yatakaposikilizwa tena. Mdee pamoja na wenzake wanane, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi na kufanya mkusanyiko …

Wapiga Kura Wamgeuka Mbunge Wao Mbele ya Waziri

SAKATA la vibali vya uvunaji miti katika msitu wa Taifa wa Sao Hill Mufindi mkoani Iringa limemuweka pabaya Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, Mendrad Kigola baada ya wapiga kura wake kumgeuka mbele ya Waziri Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa mbunge huyo ni mchochezi. Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Igowole juzi Kigola alimkaribisha waziri huyo huku akikosoa mgao wa …