Mitazamo Hasi ya Kitamaduni Yachangia Mauaji ya Albino Tanzania

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues, akiwasilisha mada katika warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kuhusu ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa dini, walimu pamoja …

Saidi Kuboresha Maisha ya Albino kwa Kupiga Kura Hii…!

SHIRIKA linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania  Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama “Tulip” itolewayo  nchini Uholanzi.  Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa  katika uboreshaji wa maisha ya watu  wenye ulemavu wa ngozi.  Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo …

Albino Aliyekatwa Mikono Awaliza Viongozi Mkutanoni

Na Mwandishi Wetu MWANAMKE albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini. Alisema hata adhabu ya kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha maisha ya mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi. Akizungumza kwa uchungu huku akitokwa na machozi kiasi cha kushidwa …