RAIS wa Marekani, Barack Obama amethibitisha wito wa kulitumia jeshi la nchi hiyo na wale wa akiba iwapo watahitajika kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika magharibi. Rais Obama amesema wanajeshi hao wataongeza nguvu ya jeshi katika kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo. Kundi la kwanza la wanajeshi hao linatarajiwa kupelekwa kusaidia ujenzi wa vituo 17 vya kutolea …
Mkuu wa Usalama Marekani Abwaga Manyanga..!
MKUU wa Idara ya Usalama nchini Marekani, Julia Pierson ambaye idara yake inahusika na kumlinda Rais wa nchi hiyo Barack Obama, ameamua kubwaga manyanga kazini baada ya shutuma kumzidia. Shutuma zilizokuwa zikimwandama zaidi ambayo huenda zimeshinikiza maamuzi ya kujiuzulu ni tukio la kuhatarisha usalama wa Ikulu ya nchini hiyo na taifa kiujumla. Bi. Pierson alikabidhi barua ya kujiuzulu kwa Waziri …
Ebola Sasa ‘Yamfuata’ Obama Marekani
IKIWA ni siku chache baada ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutangaza kutoa askari kwenda kusaidia mapambano na ugonjwa wa Ebora katika nchi zenye ugonjwa huo Afrika, Mgonjwa wa kwanza mwenye virusi vya Ebola amegundulika nchini Marekani. Taarifa zinasema mgonjwa huyo amegundulika akiwa katika Mji wa Dallas, Texas. Maofisa katika kituo cha afya cha Texas Hospitali ya Presbyterian wamesema tayari …
Rais Kikwete Awasili New York, Marekani
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Septemba 15, 2014. Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar …
Ujerumani Kusaidia Silaha Iraq, Marekani Waombwa Silaha
UJERUMANI inatarajia kupeleka silaha kwenye Jeshi la Wakurd wa Iraq zikiwemo bunduki na silaha nzito zinazoweza kutumika kushambulia kwenye vita kukabiliana na mashambulizi ya vifaru vya kivita. Jeshi hilo limekuwa likipambana na wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mwa Iraq. Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula Von der Leyen alisema silaha hizo zinauwezo wa kutumiwa na wanajeshi wapatao elfu nne ifikapo mwishoni …
Marekani Yaimwagia Lawama Misri na Falme za Kiarabu
MAOFISA nchini Marekani wamesema mataifa ya Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu zilihusika na mashambulio nchini Libya wiki iliyopita kuwalenga wanamgambo wa Kiislamu wanaopambana na vikosi vya Serikali. Ofisa mmoja Mkuu wa Marekani aliwaambia wanahabari kuwa Marekani haikushirikishwa katika mashambulio hayo na ilishangazwa. Makombora hayo yaliofyetuliwa Tripoli yanasemekana kutekelezwa na Umoja wa milki za kiarabu kwa kutumia kambi za …