KANDA moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonesha mauaji ya kinyama mfanyakazi wa huduma za misaada raia wa Marekani, Abdul Rahman Kassig ambaye anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopita. Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig …
Marekani Yatamba Kufanikiwa Mapigano na Islamic State
MKUU wa majeshi ya Marekani Generali Jack Dempsey amesema kampeni ya miezi mitatu dhidi ya dola ya kiislamu ‘Islamic State’ imekuwa na mafanikio, lakini akaeleza wazi kuwa kwa oparesheni hiyo Marekani na washirika wake walikabiliana na vikwazo kwa muda mrefu. Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Chuck Hagel aliliambia Bunge la Congress kuwa dola ya kiislamu imedhibitiwa na haiwezi kusonga …
Rais Kikwete Kuhamishiwa Hoteli Maalum kwa Uangalizi wa Madaktari
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari. Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) na …
Rais Kikwete Afanyiwa Upasuaji Marekani…!
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani. Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo. Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha …
Barack Obama Kushirikiana na Wapinzani Wake
KIONGOZI mpya wa Baraza la Senate la Marekani kutoka chama cha Republican na Rais Barack Obama wote wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani. Wanachama wa Republican wamepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi wa nusu muhula na kwa sasa wanadhibiti mabunge yote mawili nchini Marekani. Kiongozi wa baraza la Senate anayeingia madarakani Mitch McConnell amesema …