RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea huzuni na masikitiko yake makubwa kufuatia vifo vya watu 36 vilivyotokea katika ajali ya barabarani Wilayani Butiama, Mkoa wa Mara, ambako pia watu 79 wameumia, baadhi yao vibaya. Mara baada ya kupata taarifa hiyo iliyotokea, Septemba 5, 2014, Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tatu …