Mama wa ‘Wanahabari’ Kuzikwa Jumatano Mbeya

Na Joachim Mushi MAMA mzazi wa waandishi wa habari Kulwa, Dotto na Nico Mwaibale aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Hindu Mandal anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano kijijini kwao Newland (Kibunde) Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mafumu ambaye ni mama mzazi wa wanahabari Kulwa Mwaibale mwandishi wa habari wa kampuni ya Global Publishers …