Ulevi kwa Wazazi Kikwazo cha Malezi Kata ya Tembela

KITENDO cha baadhi ya wazazi kuendekeza unywaji wa pombe za kienyeji katika baadhi ya vijiji vilivyopo Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini kimesababisha wazazi hao kushindwa kuwasimamia vizuri watoto wao hasa wanafunzi jambo ambalo limesababisha kupoteza mwelekeo. Kauli hizo zilitolewa na baadhi ya viongozi wa vijiji mwishoni mwa mwaka jana walipokuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari …