Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anataka na anatamani kuwa Rais wa mwisho wa Tanzania kuongoza nchi ambayo ni maskini na hivyo atatumia muda wake uliobakia katika uongozi kuelekeza nchi kwenye mwelekeo huo. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa jambo la msingi kabisa la kama Watanzania watanufaika na ugunduzi wa gesi asili ama watabakia …