NCCR-Mageuzi; Hatujajitoa UKAWA, Wataja Majimbo Yao 19

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema taarifa zinazozagaa kuwa chama hicho kimejitoa ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) hazina ukweli wowote na kwamba hawawezi kujitoa kwa kuwa wao ni miongoni mwa waasisi wa ushirikiano huo uliozaliwa na mchakato wa Katiba mpya. Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Nderakindo …

UKAWA Wataja Mgawanyiko wa Majimbo na Vyama Vyao

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetangaza mgawanyo wa majimbo 253 kati ya 265 ya ubunge huku 12 yaliyokuwa kwenye mvutano yakibaki kiporo. Katika mgawanyo huo uliotangazwa kwa wanahabari jana, Chadema kimepata majimbo 138, sawa na asilimia 73 ya majimbo yote huku CUF ikichukua 99, NCCR – Mageuzi 14 na NLD matatu. Hiyo ni pamoja na kujumlisha majimbo …