Waziri Pinda Afunga Michezo ya Majeshi Afrika Mashariki

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hayana budi kuendeleza umoja na mshikamano ili kukuza udugu uliopo. Ametoa kauli Agosti 29, 2014 wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.   Waziri Mkuu ambaye kabla ya kuhutubia umati ulioshiriki …