Mahakama Afrika Kuanza Kikao Jumatatu Arusha

Na Mtuwa Salira, EANA MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) inaanza kikao chake cha kawaida cha 36 cha mwaka, kuanzia Machi 9 hadi Marchi 27, mwaka huu, katika makao yake makuu mjini Arusha, Tanzania. Majaji wa mahakama hiyo pamoja na mambo mengine watapokea na kujadili taarifa za mikutano miwili ya kawaida iliyopita na maombi mengine yaliyokwishawasilishwa …