Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi

Mahakama Zamkera JPM, ni Kuhusu Kesi za Ukwepaji wa Kodi RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na namna Mahakama inavyoshughulikia kesi zinazohusiana na ukwepaji wa kodi na ametoa wito kwa mahakama na wadau wake kujipanga kukabiliana na dosari hiyo inayorudisha nyuma juhudi za maendeleo ya nchi. Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli …

Rais Magufuli Akamilisha Ahadi Aipa Mahakama Bilioni 12.3

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO SERIKALI imeikabidhi Mahakama ya Tanzania kiasi cha Sh. bilioni 12.3 zilizoahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria kwa lengo la kuiwezesha Mahakama kuimarisha utendaji kazi na kutekeleza majukumu yake inapasavyo. Akikabidhi fedha hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, …

Watuhumiwa Escrow Mahakamani, CCM Kuwajibisha Makada

WAKATI Serikali ya Tanzania imeanza kuwafikisha mahakamani baadhi ya maafisa wanaotuhumiwa kuhusika na gawio la fedha kutoka akaunti ya Tegeta ESCROW, Chama tawala nchini humo CCM, kimetoa kauli ya kuwachukulia hatua, makada wake wanaohusishwa na kashfa hiyo. Suala la kashfa ya akaunti ya mabilioni ya fedha yaliyochotwa kutoka akaunti ya Tegeta Escrow, si tu imekichafua chama tawala nchini humo kutokana …

Mahakama Kupunguza Muda wa Mashauri Kukaa Mahakamani

Na Georgina Misama – MAELEZO MAHAKAMA ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote ili kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na rufaa kukaa Mahakamani kwa muda mrefu. Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Mary Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Akizitaja hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha …

Mahakama Yamfunga Jela Mwizi wa Nyaya za TTCL

Na Mwandishi Wetu MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam imemuhukumu kwenda jela miaka minne, Shaibu Muhidin Ndina baada ya kupatikana na kosa la kuiba nyaya za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Hukumu hiyo imetolewa Agosti 25, 2014 katika mahakama hiyo na B. Mashabara baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa hilo la wizi wa nyaya(cables) za …