Mpambano Mkali wa Ngumi Kufanyika Oktoba 25

Mwandishi Wetu MPAMBANO mkali wa mchezo wa masumbwi utakaowakutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania unatarajia kufanyika Oktoba 25, 2014 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es Salaam. Akizungumzia mpambano huo Mratibu wa pambano hilo ambaye pia ni kocha wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema maandalizi yanaendelea vizuri. Alisema kuwa siku hiyo kutakuwa …