Rais Obama Kutumia Jeshi Kupambana na Ebola Afrika

RAIS wa Marekani, Barrack Obama ametangaza mpango wake wa kuwatuma wanajeshi 3,000 Afrika Magharibi kama njia mojawap ya kusaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola. Rais Obama ametoa kauli hiyo huku akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika ambao unaenea kwa kasi sana. Bwana Obama amesema …