Mpango wa Kukuza Stadi za Kusoma Wazinduliwa, KKK

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amezindua Mpango wa Kitaifa wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaolenga kukuza viwango vya uelewa kwa watoto wa darasa la kwanza na la pili kwa nchi nzima.   Mpango huo wa miaka mitatu ulioanza kutekelezwa 2014/2015 hadi 2016/2017 umelengwa kuwahusisha watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 13 walio kwenye mfumo rasmi …