Rais Kikwete Kurejea Dar Kesho

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kurejea nchini Tanzania kesho majira ya mchana, Novemba 29, 2014 kutoka kwenye matibabu nchini Marekani. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu; imesema Rais Kikwete atawasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates saa 9:20 mchana. …