Kipindupindu Charejea Dar, Chaibukia Kigamboni

Na Dotto Mwaibale WAKATI jiji la Dar es Salaam likiwa katika  mapambano ya kukabiliwa na dawa za kulevya jiji hilo limekumbwa na ugonjwa wa kipindupindu ambapo mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Ramadhan Kiumbo (maarufu kwa jina la Popo) mkazi wa Kibada Kigamboni amefariki kutokana na ugonjwa huo.   Akizungumza Dar es Salaam leo ndugu yake na marehemu huyo aliyejitambulisha …

Ubalozi wa Kuwait Tanzania Wasaidia Kambi ya Kipindupindu Zanzibar

    Madawa na Maji vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini TanzaniaBalozi  Jasem Al-Najem, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya Kambi za Kipindupindu Zanzibar. Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, akisalimiana na Daktari Kanda ya Unguja, Dk Fadhil Mohammed wakati wa hafla ya kukabidhi Madawa na Maji kwa ajili ya Kambi za Kipindupindu Zanzibar. Balozi Jasem Al-Najem, akizungumza na …

Waziri Ummy Mwalimu Atembelea Kambi ya Kipindupindu Geita

Wananchi wa Mkoa wa Geita wametakiwa kufuata kanuni za usafi wa mazingira ili kudhibiti maumbukizi ya ugonjwa wa kipindupindu, Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya cha Nyankumbu, mkoani hapa Waziri Ummy akivua vifaa hivyo mara baada ya kutoka kuwasalimia …

Kipindupindu Chaendelea Dar, Wagonjwa Wafikia 43

 Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Nusura Kessy (kushoto), akiwaelekeza wauguzi wa saidizi wake namna ya kuchanganya dawa maalumu ya kuondoa vijiji vinavyoweza kuambukiza ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi. Katika kambi hiyo kuna wagonjwa 21 kati yao watoto ni 7.  Vyombo vikiwekwa kwenye dawa. Dawa …

Kipindupindu Chaibuka Dar, Chauwa Wawili Kinondoni

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq ametoa tahadhari kwa wakazi wa jiji hilo kuwa makini kwani ugonjwa wa kipindupindu tayari umevamia baadhi ya maeneo ya jiji. Mkuu huyo wa mkoa alisema tayari watu 24 wamelazwa baada ya kubainika kuwa na ugonjwa huo, huku watu wengine wawili (mwanamke na mwanaume) wameshapoteza maisha kwa ugonjwa huo. Alisema taarifa …

Kipindupindu Chawatesa Wakimbizi wa Burundi Tanzania

UMOJA wa mataifa unasema kuwa zaidi ya visa 400 vya ugonja wa kipindupindu vinaripotiwa kila siku miongoni mwa wakimbizi wa Burundi walio nchini Tanzania. Maelfu ya watu wamewasili kwa mashua wakikimbia ghasia za kisiasa nchini Burundi Wamechukua hifadhi katika sehemu zenye misongamano na zilizo na mazingira mabaya. Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban watu 3000 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu na …