Idadi ya Watalii Wanaotembelea Kilimanjaro Waongezeka

IDADI ya watalii wanaotembelea hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) imeongezeka kutoka 37,000 hadi kufikia 51,287 ndani ya kipindi cha miaka 10 huku asilimia 4 na sita kati yao wakiwa ni wazawa. Asilimia hiyo inatajwa ni ya watanzania ambao wamekuwa wakipanda Mlima huo kwa muda wa siku moja hali inayoilazimu uongozi wa hifadhi hiyo kuendelea kuhamsisha wananchi kutembelea hifadhi …

Matukio Katika Picha Sherehe za Mei Mosi Mkoani Kilimanjaro

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme(TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro wakipita na gari lao mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu chaUshirika  mjini Moshi.  Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipita katika maonesho ya Mei Mosi Mkoani Kilimanjaro. Chuo cha wauguzi Kibosho pia walipita mbele ya mgeni rasmi kuonesha nini wanafanya katika sherehe hizo za …

NSSF Washiriki Mbio za Kilimanjaro Marathon

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki kwenye Mbio za nyika za zinazoendelea kuwa maarufu mwaka hadi mwaka Kilimanjaro ambazo zimefanyika kwa mwaka wa 13 mfululizo. NSSF ilishiriki ikiwa kama mdhamini wa mbio za KM 5 ambazo zilishirikisha washiriki zaidi ya 3500. Pamoja na udhamini huo NSSF ilipata nafasi ya kutoa elimu kwa wakazi mbalimbali wa Mkoa wa …

Viongozi wa Chadema Wampinga Mkuu wa Mkoa

KAULI ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama ya kuwataka viongozi wa serikali za vijiji kuondoka katika ofisi walizokua wakizitumia awali na kwenda kupanga majengo ya watu binafsi imepingwa vikali na wananchi pamoja na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kauli ya Mkuu wa mkoa aliitoa Februari 5, 2015 wakati alipokua akizungumza na viongozi wa kata, vijiji na …