FAMILIA ya Bwana William H. Shelukindo, Inasikitika kutangaza kifo cha Bibi Beatrice Matumbo Shelukindo kilichotokea siku ya Jumamosi 2/7/2016 huko Arusha. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu 8 Galu Street, Ada Estate, Dar es salaam na huko Arusha. Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano Tarehe 6/07/2016 alasiri Mjini Arusha. Bwana ametoa Bwana, ametoa Jina la Bwana lihimidiwe.
Padre Awataka Waumini Kujiweka Tayari kwa Kifo…!
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam PAROKO wa Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa, Padre Ephraim Ogha amewataka Watanzania na hasa waumini wa Kanisa Katoliki kujiweka tayari wakati wowote na kifo kwani kila mmoja atafikwa na tukio hilo kwa wakati wake. Paroko Ogha alitoa tahadhari hiyo alipokuwa akihubiri katika ibada maalumu ya kumuombea aliyekuwa mwandishi wa habari …
Waziri Pinda Ataka Watanzania Kuandika Wosia Kabla ya Kifo
Na Mwandishi Maalum WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amewataka Watanzania wote nchini wajenge tabia ya kuandika wosia ili kuondoa matatizo ya mirathi pindi mume anapoaga dunia. Ametoa wito huo Mei 29, 2015 wakati akizindua kampeni ya kuandika wosia kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. …
Tanzania Yatuma Rambirambi Kifo cha Rais Zambia
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameshtushwa na kusononeshwa sana na taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Zambia, Michael Chilufya Sata ambacho kimetokea jana, Jumanne, Oktoba 28, 2014 kwenye Hospitali ya King Edward VII, London, Uingereza, ambako alikuwa anatibiwa akiwa na umri wa miaka 77. Katika salamu ambazo amempelekea Makamu wa Rais wa Zambia, Mheshimiwa …
Ikulu Yatuma Rambirambi Kifo cha Dk Shija
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameelezea huzuni na masikitiko yake kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuia ya Madola (CPA), Dk. William Shija. Dk. Shija aliyefariki dunia Jumamosi asubuhi mjini London, Uingereza, ambacho ndicho kilikuwa kituo chake cha kazi, alisomea na kuwa mhadhiri wa uandishi wa habari kabla ya …
Mwanahabari Alfred Ngotezi afariki
TASNIA ya habari Tanzania imepata pigo kubwa baada ya jana kundokewa na mwandishi wa habari mkongwe, Alfred Ngotezi. Taarifa zilizopatikana jana usiku zinaeleza kuwa Ngotezi, alidondoka muda mfupi baada ya kutoka maliwato, akiwa katika moja ya hoteli za Mji wa Arusha na alifariki dunia muda mfupi baadaye. Inaelezwa kwamba alifariki saa 5:11 usiku “Ndugu yetu baada ya kurejea kutoka maliwatoni, …