Na Frank Mvungi-Maelezo SERIKALI imedhamiria kuendelea kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayowasilishwa ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Aidha, Mwakapeje amesema Wizara hiyo imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusu ucheleweshwaji wa …