NDEGE za kivita za Jeshi la Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Al-shabaab katika taifa jirani la Somalia, taarifa kutoka jeshi hilo zimesema. Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya Jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza. Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya. Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka …
Kenya, Tanzania Wamaliza Mvutano wa Marufuku…!
HATIMAYE marais Uhuru Kenyetta wa Kenya na Jakaya Kikwete wa Tanzania wamekubaliana kufutilia mbali maagizo ya Mamlaka ya anga nchini Tanzania kupunguza idadi ya ndege za Kenya zinazotua nchini Tanzania na agizo la Wizara ya maliasili ya Kenya kupiga marufuku magari ya Tanzania kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Katika makubaliano hayo ndege za Kenya Airways sasa zitafanya …
Beach Soccer; Tanzania Kuivaa Kenya, Twiga Kutinga Kambini
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) kesho jumamosi itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo utakaoanza majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Escape One Club Msasani jijini Dar es salaam. Wageni timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni kutoka nchini Kenya wanatarajia kuwasili leo jioni jijini …
Kenya Yaruhusu Magari ya Watalii Tanzania Kuingia Jomo Kenyatta
Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema Serikali ya Kenya imekubali kuyaruhusu magari ya abiria na watalii kutoka Tanzania, kuingia ndani ya Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Awali, Serikali ya Kenya iliyazuia magari hayo kuingia uwanjani hapo huku ukiyatoza ushuru kwa yale yanayoingia, jambo ambalo lililalamikiwa na wafanyabiashara wa Tanzania. Zuio hilo la Kenya kwa magari ya …
Kenya Wavamia Kambi ya Al-Shabaab, Waua Wapiganaji 100
MAKAMO wa Rais wa Kenya, William Ruto, amesema kuwa askari wa usalama wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa Al-Shabaab hadi kwenye kambi yao nchini Somalia, baada ya shambulio dhidi ya basi Kaskazini – Mashariki mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28 wa Kenya waliuliwa. Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 wa kundi la Al-Shabaab waliuliwa katika operesheni mbili tofauti zilizofanywa na …
Sauti Sol wa Kenya Ndani ya Beauty na Music Night
Kundi la muziki kutoka nchini Kenya Sauti Sol waking’ara kwenye Red Carpet mwishoni mwa juma kwenye BEAUTY and MUSIC Night uliofanyika kwenye fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar. Petit Man (katikati) akishow love na wasanii wa bongo flava waliotumbuiza kwenye usiku huo maalum Kulia ni Mirror na Kushoto ni msanii wa bongo flava Jordan. Mwanadada mrembo akishow love mbele …