Katibu Mkuu Coastal Union Kushtakiwa TFF

KATIBU Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi atafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushinikiza mkutano wa wanachama wa klabu hiyo ufanyike bila kuandaliwa na Kamati ya Utendaji.   Pia El Siagi alitumia vyombo vya habari kuishambulia TFF ambayo haikutambua uamuzi wa mkutano huo ulioelezwa kumdumaza Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Steven …