JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKATA) limeitaka Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli kufufua mchakato wa Katiba Mpya ambao limedai ulitelekezwa kimya kimya bila maelezo ya kueleweka. Mwenyekiti wa JUKATA, Deus Kibamba akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam katika ofisi zao ameitaka Serikali kufufua mchakato huo na kuanzia na kuitisha mkutano mkuu maalumu …
Watanzania Kupiga Kura ya Maoni Katiba Mpya Aprili 2015
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kuwa endapo mipango yote itakwenda kama inavyoandaliwa, Watanzania watapata nafasi ya kuipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa, ili kukamilisha mchakato wa Tanzania kusaka Katiba Mpya. Rais Kikwete amesema hayo Oktoba 22, 2014, wakati alipokutana na kuzungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China. Mkutano huo na …
JK Asema Katiba Inayopendekezwa ni Historia Mpya…!
Na Benedict Liwenga, Maelezo – Dodoma KATIBA Inayopendekezwa imekabidhiwa rasmi 8 Oktoba, 2014 kwa Waheshimiwa Marais wa Tanzania Bara, Dk. Jakaya Kikwete pamoja Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein. Akihutubia wakati wa sherehe ya Makabidhiano ya Katiba hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mrisho Kikwete alisema kuwa tukio hilo ni jambo la kihistoria kwa nchi ya …
Cheyo Awataka Watanzania Wasidanganyike Kuhusu Katiba
Na Benedict Liwenga, MAELEZO – Dodoma MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo amewataka Watanzania kutodanganywa kuhusiana na mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya. Kauli hiyo imetolewa na Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha asubuhi cha Jambo kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Habari Tanzania (TBC). Cheyo amesema kuwa …
Wanawake Wataka Katiba Mpya Itamke Umri wa Kuolewa, Kuoa
Na Mwandishi Wetu, Dodoma WANAHARAKATI wanaoshiriki kongamano la Katiba la kujadili masuala ya kijinsia yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye mjadala wa Bunge maalum la Katiba wamewataka wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kuhakikisha katiba mpya itakayotengenezwa inatamka umri wa kuolewa au kuoa uwe miaka 18 hadi 21 ili kuwapa nafasi watoto wa kike kupata nafasi ya kusoma na kukua. Wakizungumza wakati wakiendesha Bunge kivuli …
Sitta Asema Katiba Mpya Itakayopatikana Itakuwa Bora
Na Magreth Kinabo na Rose Masaka MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta amewahakikishia Watanzania kwamba Katiba Mpya itakayopatikana itakuwa imezingatia matakwa ya makundi mbalimbali. Sitta aliyataja makundi hayo kuwa ni wafugaji, wakulima, wavuvi na wasanii. Huku akisema Katiba Mpya itakayopatikana itakuwa ni bora kuliko ya iliyopo sasa. Kauli hiyo ilitolewa na Sitta wakati akizungumza na wafugaji wapato 44 kutoka …