Taasisi za Umma Marufuku Kujenga Vituo Binafsi vya Kuifadhi Data

                SERIKALI imezitaka taasisi zake kote kuachana na mpango wa kujenga Vituo binafsi vya vya kuhifadhia kumbukumbu (Data Center) na badala yake kutumia Kituo cha Serikali cha kuhifadhia Data na kumbukumbu (NIDC) chenye uwezo na hadhi ya Kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa baada …

Chuo cha CBE Waibuka Vinara ‘TTCL Inter College Beach Soccer’

    Na Mwandishi Wetu CHUO cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE) kimeibuka vinara wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni ‘TTCL Inter College Beach Soccer’ yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kupitia kocha wa taifa wa mpira huo wa ufukweni nchini. Chuo cha …

Kampuni ya TTCL yadhamini michuano ya vyuo Soka la Ufukweni

Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa tatu kushoto) akimkabidhi nahodha wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), Ally Rabi (wa tatu kulia) fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa …

Makonda Azitaka Taasisi na Mashirika ya Umma Kutumia Huduma za TTCL

          MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka taasisi na mashirika ya umma yaliopo chini ya mkoa wake kuiunga mkono Kampuni ya Simu ya kizalendo Tanzania (TTCL) kwa kuanza kuzitumia bidhaa za kampuni hiyo hasa kwenye shughuli za mawasiliano ili kuonesha uzalendo kwa vitendo. Makonda ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya TTCL …

Mtendaji Mkuu Mpya wa TTCL Atembelea Ofisi Yake

  KAIMU Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba, leo ametembelea Makao Makuu ya TTCL na kukutana na Mtangulizi wake, Dk. Kamugisha Kazaura. Utambulisho wa awali wa kiongozi huyo mpya umefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, anaesimamia sekta ya Mawasiliano Prof Faustine Kamuzora. Makabidhiano rasmi ya ofisi yatafanyika baadae.   …