Mama Samia Suluhu Atembelea Wagonjwa Huruma Hospitali, Ahaidi Kuboresha Huduma

Na Joachim Mushi, Moshi MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ametembelea Hospitali ya Huruma ya Wilaya ya Rombo na kusikiliza changamoto anuai zinazowakabili wagonjwa hospitalini hapo kabla ya kufanya mkutano wa hadhara kuinadi ilani ya CCM, huku akiahidi kuendelea kuboresha huduma za afya endapo CCM itachaguliwa tena na kuunda serikali katika uchaguzi …