Dk. Magufuli ‘Aunguruma’ Uwanja wa Tangamano Tanga…!

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli akifafanua jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Tanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jioni ya Mjini Tanga.   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa …

Mama Samia Atuwa Mkoani Ruvuma, Ainadi Ilani ya CCM Majimbo Mawili

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambugu (kulia) alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ruvuma leo kabla ya kuanza ziara ya mikutano ya kampeni kunadi ilani ya chama hicho mkoani hapo. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha …

Tutadhibiti Wizi wa Dawa Hospitali za Serikali- Samia Suluhu

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema Serikali watakayoiunda endapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi watahakikisha wanadhibiti wizi wa dawa kwenye hospitali za Serikali ambazo zimekuwa zikiuziwa wananchi katika maduka ya dawa mitaani. Bi. Suluhu katoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia katika mikutano ya anuai ya …

Mgombea Mwenza Urais CCM Ahaidi Neema kwa Wajasiliamali Dar

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu amesema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetenga kiasi cha fedha kitakachotumika kama dhamana ili wajasiliamali mbalimbali wa jijini Dar es Salaam waweze kudhaminiwa kwenye mabenki na kupewa mikopo ili kuendeleza biashara zao. Bi. Samia amesema hayo leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa …

CCM Kuja na Muarobaini Mapigano ya Wafugaji na Wakulima

Na Joachim Mushi, Dodoma MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi Okuu wa Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi. Bi. Suluhu ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilaya ya CCM katika Majimbo mawili …

Mgombea Ubunge CCM Kawe Azinduwa Kampeni Dar

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia) akimtambulisha Mgombea …