JK Amteuwa Dk. Moses Kusiluka Kamishna Ardhi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dk. Moses Mpogole Kusiluka (42) kuwa Kamishna Ardhi nchini. Uteuzi huo ulianza Jumanne ya Desemba 23, mwaka huu, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Dk. Kusiluka alikuwa Mkuu wa Idara ya Real Estate Finance and Investment katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam, ambako amekuwa mhadhiri kwa miaka minane …