JK: Asilimia 90 ya Watoto Wanapata Chanjo Tanzania, Apewa Tuzo Ujerumani

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kuwa asilimia 90 ya watoto wote Tanzania sasa wanapata chanjo kutokana na kazi inayofanywa na taasisi ya kusambaza chanjo duniani ya Global Alliance for Vaccines and Immunisazation (GAVI). Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa bila kazi hiyo ya GAVI ni dhahiri kuwa baadhi ya nchi duniani hasa zile zinazoendelea zingekuwa zinapoteza …

JK Amteuwa Dk. Moses Kusiluka Kamishna Ardhi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dk. Moses Mpogole Kusiluka (42) kuwa Kamishna Ardhi nchini. Uteuzi huo ulianza Jumanne ya Desemba 23, mwaka huu, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Dk. Kusiluka alikuwa Mkuu wa Idara ya Real Estate Finance and Investment katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam, ambako amekuwa mhadhiri kwa miaka minane …

JK Awapasulia Watumishi wa Umma Tanzania

Na Mwandishi Maalum, RAIS Jakaya Kikwete amewataka watumishi wa umma nchini kubadilika katika utendaji wao ili kuwa wawezeshaji zaidi badala ya wakwamishaji katika kutoa maamuzi yanayopelekea utendaji wa shughuli mbalimbali nchini. Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. “Watu wanaona utumishi wa Umma …