Mambo Yaharibika Bukina faso Jeshi Lapindua Nchi

AMIRI Jeshi Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso, Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge la nchi. Kiongozi huyo mkuu wa jeshi hata hivyo hakuweka wazi ni nani atakayeshikilia uongozi wa taifa hilo kwa sasa. Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi aliyepinduliwa …