Insignia Limited Yapata Cheti cha Mazingira cha ISO 14000

KAMPUNI inayoongoza kwa uzalishaji wa rangi nchini Tanzania ya Insignia Limited, inajivunia kutangaza kupata cheti cha ISO 14000, cheti cha kiwango cha kimataifa cha uwajibikaji katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira. Viongozi wa kampuni walitangaza mafanikio hayo mjini Dar es Salaam. Cheti hicho cha ISO kilitolewa kuthibitisha viwango vya kampuni kufwatia dhamira yake katika shughuli za utunzaji wa mazingira. Mwaka …