Imetosha Foundation Watembelea Kituo cha Buhangija Shinyanga

Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu …

Imetosha Foundation Waelekea Mwanza Kuandaa…!

  Balozi Henry Mdimu akiongea na vyombo vya habari Taasisi isiyo ya ki serikali ya Imetosha Foundation inayopinga unyanyapaa, ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu, inatarajia kutuma ujumbe mzito kanda ya ziwa hapo kesho kwa maandalizi ya ujio wa timu nzima ya taasisi hiyo iliyojikita kwenye kubadilisha mtazamo (mind set) wa watu juu ya …