Halima Mdee Apelekwa Segerea, Akosa Dhamana

MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (35), jana alikosa dhamana na kupelekwa rumande katika Gereza la Segerea hadi leo maombi ya dhamana yake yatakaposikilizwa tena. Mdee pamoja na wenzake wanane, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi na kufanya mkusanyiko …